Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Inspekta Haroun amefunguka na kueleza sababu mbalimbali zinazowafanya wasanii wakongwe kushindwa kufanya vizuri kama zamani.
Inspekta amesema hakuna ugumu kwa msanii mkongwe kufanya vizuri katika kipindi hiki ila muziki wao umekuwa na changamoto kadhaa.
Mwanamuziki huyo amesema kuwa “Muziki hauna mipaka kusema huyu mkongwe huyu wa sasa, yaani hata mimi leo nikiandaa ngoma yangu nzuri pamoja na video nitarudi vizuri tu. Unatakiwa uandae kitu kuanzia chini, watu wanataka kutengeneza tu video kali no, zalima audio iwe kali ili video ije kufanya vizuri zaidi,”.
Inspekta aliongeza kwa kusema kuwa , “Mashabiki wa muziki ni wale wale, wapo wanaopenda bongo fleva ya sasa hivi na wapo wanaopenda bongo fleva ya zamani, kwa hiyo haijalishi ukifanya kitu kizuri uwe mkongwe uwe mwanamuziki wa sasa utasimama.
Miezi michache iliyopita Inspekta Haroun alidai kuwa alianza kufikiria biashara nyingine ya kufanya baada ya kutoa nyimbo takriban 20 na zote zikapotea hivi hivi, lakini baadaye alifanyiwa cancelling na familia yake nakurudi tena katika mapigano.
Inspekta Horoun aliwahi kutamba miaka ya nyuma wakati akiwa kundi la Gangwe Mob kutoakana na nyimbo zake kama ‘Mtoto wa gheto kali’.