Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limesema Shindano la Dance100% lililomalizika Jumamosi katika viwanja vya Don Bosco Jijini Dar es salaam limewafanya vijana kuwa wamoja na kujenga urafiki.

Mkuu wa Matukio kutoka BASATA Kurwijira N Maregesi amesema hayo wakati alipokuwa akitoa tathmini yake kuhusu namna shindano la Dance100% lilivyofanyika mwaka huu kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Maregesi ameongeza kuwa licha ya mbali umoja ambao umejengeka baina ya makundi ila wengine wanaweza kujipatia ajira kwani shindano hilo limetazamwa na watu wengi na wasanii ambao wanaweza kutaka wachezaji katika kazi zao pamoja na kushiriki shughuli mbalimbali za kitaifa na za kijamii.

Shindano la Dance100% limemalizika kwa kundi la Team Makorokocho kuibuka kidedea na kuondoka na kitita cha milioni 7 wakifuatiwa na kundi la J Combat kutoka Zanzibar ambao wameibuka na kitita cha milioni mbili na kundi lililoshika nafasi ya tatu ni D.D.I Crew ambao wamejipatia shilingi milioni moja.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *