Kampuni ya Samsung imechelewesha uuzaji wa simu aina ya galaxy Note 7 nchini Korea Kusini kwa sababu kampuni hiyo inahitaji muda zaidi wa kuzirudisha simu kama hizo ambazo zilikuwa na matatizo ya betri.

Kampuni hiyo ya teknolojia nchini Korea Kusini ililazimika kuzirudisha takriban simu milioni 2.4 kutokana na betri zilizokuwa zikilipuka.

Simu hiyo ilitarajiwa kurudishwa madukani Septemba 28 lakini sasa inatarajiwa kurudi madukani Oktoba mosi mwaka huu ikiwa ndio mapema zaidi.

galaxy-note-7-20

Mnamo Septemba 2, Samsung ilikuwa imesema itaacha kuuza simu hizo na kuomba kurudisha simu ambazo zilikuwa imeuza.

Kampuni hiyo pia iliwataka walionunua simu hizo kuwacha kuzitumia ktokana na matatizo hayo kuwa makubwa sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *