Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi atakuwa nje kwa wiki tatu kufutia kuumia nyonga kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uhispania dhidi ya Atletico Madrid iliyofanyika katika uwanja wa Nou Camp na matokeo kumalizika 1-1.
Messi alitoka nje dakika ya 59 baada ya kugongwa na mlizi wa Atletico Madrid, Diego Godin kwenye mechi hiyo iliyofanyika jana usiku.
Mshambuliaji huyo alikosa mechi ya kufuzu ya kombe la dunia kati ya Argentina na Venezuela mapema mwezi huu kutoka na majeruhi lakini alifanikiwa kurudi uwanjani na kucheza mechi tato za La Liga kaba ya kuumia tena jana.
Messi atakuwa nje katika mechi dhidi ya Borussia Monchengladbach kwenye klabu bingwa, Sporting Gijon and Celta Vigo kwenye La Liga na mechi ya kufuzu kombe dunia dhidi ya Peru na Paraguay.
Mshambuliaji huyo anatarajiwa kurudi uwanjani kwenye mechi ya klabu bingwa kati ya Barcelona na Manchester City itakayofanyika Oktoba 19 mwaka huu.