Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameagiza fedha zilizookolewa katika malipo ya posho zisizo halali kwa madiwani zitumike kuwalipa madeni walimu wa shule za msingi na sekondari mkoani humo.
Gambo ametoa agizo hilo wakati wa kikao kilichowajumisha walimu wa shule za msingi na sekondari kilichofanyika mkoani Arusha na kutaja kiasi cha fedha hizo kuwa ni shilingi milioni 150.
Mkuu wa mkoa huyo ametoa kauli hiyo mara baada ya walimu kulalamikia madeni yao pamoja na posho za mazingira magumu bila kupata msaada wowote, hivyo kumuomba mkuu huyo wa mkoa kuingilia kati.
Gambo ametoa wiki mbili kwa mkurugenzi wa jiji la Arusha kuhakikisha analipa madeni yote ya walimu hao na wenyewe wawasiliane na serikali kuu kujua ni jinsi gani wataweza kupata pesa zao.