Kiungo wa Tottenham, Dele Alli amesaini mkataba mpya kwenye timu hiyo ambapo utamuwezesha kubakia mpaka msimu wa mwaka 2022.
Dele Alli mwenye umri wa miaka 20 ameungana na wachezaji wenzake waliosaini kubaki Spurs ambao ni Christian Eriksen, Eric Dier, Harry Winks naTom Carroll huku Danny Rose, Jan Vertonghen na Erik Lamela wakiwa katika mazungumzo juu la mikataba mipya.
Kiungo huyo alijiunga na Tottenham msimu uliopita akitokea klabu ya MK Dons inayoshiriki ligi ya Champiship ambapo hadi sasa ameshinda magoli 10 toka ajiunge na wakali hao wa White Hart Lane.
Kiwango chake kilimfanya kiungo huyo atwae tuzo ya mwanasoka bora kijana msimu uliopita na mpaka kupelekea kuitwa kwenye timu ya taifa ya Uingereza ambapo yupo hadi sasa kwenye timu hiyo.
Vile vile kiungo huyo alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Uingereza walioshiriki kombe la mataifa ya Ulaya ambapo walifungwa hatu ya robo fainali na timu ya taiafa ya Island na kutolewa kwenye michuano hiyo.
Baada ya kusaini mkataba huo kiungo huyo amesema kuwa anajisikia furaha sana kuendelea kubakia kwenye klabu hiyo na anawashukuru mashabiki wa Tottenhama kwa kuwaunga mkono kwenye mbio za ubingwa wa Uingereza pamoja na Ulaya.