Mwanamuziki mkongwe wa miondoka ya kwaito nchini Afrika Kusini, Mduduzi Tshabalala ‘Mandoza’ amefariki akiwa na umri wa miaka 38 baada ya kuugua saratani kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Mandoza alisifika kwa albamu kadha za muziki aina ya Kwaito, aina ya muziki wa Afrika Kusini ambao hukaribiana sana na Hip Hop.
Nyimbo zake nyingi sana zilivuma, zikiwemo nyimbo kutoka albamu yake ya kwanza Nkalkatha, Godoba na Sgelekeqe .
Familia ya Mandoza imesema mwanamuziki huyo aligunduliwa kuwa na saratani baada ya kuanza kuumwa na kichwa sana pamoja na kutatizwa na macho mwaka mmoja uliopita.
Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma ametuma salamu za rambi rambi kufuatia kifo cha mwanamuziki huyo muanzilishi wa Kwaito nchini Afrika Kusini.