Rais wa Shirikisho la soka  nchini TFF, Jamal Malinzi amempongeza Alexander Ceferin kuchaguliwa kuwa Rais Mpya wa Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) katika uchaguzi mkuu uliofanyika Septemba 14 mwaka huu.

Rais Malinzi ameelezea kuwa kuchaguliwa kwa Ceferin ambaye ni Rais wa Chama cha Soka Slovakia ni kilelelezo cha familia ya mpira wa miguu ya Ulaya kuona umuhimu wake katika kutumikia shirikishi hilo sambamba na kuwa kiongozi wa FA ya Slovekia.

Rais Malinzi amesema ana imani na Ceferin kuwa ataweza kutumikia vema nafasi zote huku akisema ana imani Caferin ataunganisha nguvu kwa maendeleo ya soka kwa kushirikiana na Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Gianni Infantino na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Issa Hayatou.

Coferen: Rais mpya wa UEFA
Coferin: Rais mpya wa UEFA

Ceferin amechaguliwa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Michel Platini ambaye alifungiwa na FIFA kwa miaka minane Baada ya kukutwa na kosa la kupokea rushwa ya Pauni 1.3mil.

Rais huyu mpya alimshinda Michael Van Praag Rais wa chama cha mpira cha Uholanzi katika kura zilizopigwa huko Athens.

Ceferin atashika kiti hicho cha uraisi mpaka mwaka 2019.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *