Rais wa zamani wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva amefunguliwa mashtaka ya rushwa na wizi wa fedha wakati akiwa rais wa nchi hiyo ambapo amefunguliwa mashtaka hayo pamoja na mke wake.
Mwendesha mashtaka wa seriakali Deltan Dallagnol amesema kuwa Lula alikua kinara wa rushwa na kashfa ya kampuni ya kickback inayomilikiwa na serikali Petrobras ambayo ilikua na nia ya kuwaacha wafanyakazi wake serikalini.
Lula anashukiwa pia kukubali nyumba ya kifahari katika ufukwe wa Guaruja kutoka kwa kampuni ya ujenzi iliyopewa mkataba kipindi yeye yupo madarakani.
Wanasheria wa Rais huyo wa zamani wamesema kuwa hakuna ushahidi wowote wa madai hayo.
Chini ya sheria ya Brazil hakimu ataamua kukubali au kukataa kupokea mashtaka hayo ndani ya siku zijazoyo.