Kiungo wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil na klabu za PSG, Barcelona na AC Milan, Ronaldiho Gaucho ametangaza kustaafu soka kwa ujumla mwishoni mwa msimu baada ya kudumu kwenye mchezo huo kwa miaka 18.
Ronaldinho amesema kwasasa umri wa miaka 36 alionao unatosha kupumzika kwani mwili wake sasa unahitaji kupumzika na kuangalia mambo mengine na si masuala ya mpira tena.
Staa huyo alitamba na timu ya taifa ya Brazil katika mashindano mbali mbali ya kimataifa na jina lake lilipata umaarufu katika michuano ya kombe la dunia nchini Korea Kusini na Japan mwaka 2002.
Kwenye michuano hiyo Ronaldinho alipata umaarufu kwa kuonesha kiwango cha hali ya juu kwenye mechi ya robo fainali kati ya Brazil na Uingereza baada ya kushinda goli la faulo ya mbali na kumshinda golikipa wa Uingereza wakati huo David Simeni.
Ronaldinho alijiunga na Barcelona mwaka 2003 akitokea klabu ya PSG ya Ufaransa ambapo alisajiliwa na kocha wa wakati huo Frank Rijkard ambapo Gaucho aliifanya timu hiyo kuwa bora na kuanza kupata mashabiki duniani kote.
Ronaldinho kwasasa ni balozi wa klabu ya Barcelona ambayo aliichezea kipindi akiwa Ulaya ambapo alifanikiwa kushinda kombe la La liga, UEFA ligi pamoja na kombe la mfalme.
Pia Gaucho amefanikiwa kushinda kombe la dunia mwaka 2002 akiwa na Brazil ambapo walifanikiwa kuifunga Ujeruamni goli 2-0 wakati huo chini ya kocha Scolari.