Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amerudisha pesa zilizotumiwa kukarabati nyumba yake binafasi jinsi ilivyoamriswa na mahakama.

Msemaji wa wizara ya fedha amethibitisha kuwa pesa hizo zimepokelewa katika wizara hiyo.

Wizara ya fedha nchini Afrika Kusini ilikuwa imependekeza kuwa Rais Zuma alihitajika kurejesha dola 509,000 kwa serikali, pesa zilizotumiwa kukarabati nyumba yake huko Nkandla.

Mahakama ya juu zaidi nchini humo ilikuwa imetoa uamuzi mapema mwaka huu, kuwa Zuma alipe dola milioni 23 pesa za umma zizotumiwa kwa nyumba yake mwaka 2009.

NKANDLA: Muonekano wa nyumba ya Zuma aliyoijenga kutokana na pesa za umma ambapo ameamuriwa na mahakama kuzirejesha pesa hizo.
NKANDLA: Muonekano wa nyumba ya Zuma aliyoijenga kutokana na pesa za umma ambapo ameamuriwa na mahakama kuzirejesha pesa hizo.

Sakata ya Nkandla ilitishia wadhifa wake Zuma. Alikwepa hatua ya kumuondoa madarakani na shinikizo za kumtaka ajiuzulu.

Hata hivyo aliomba msamaha kwa njia ya runinga mwezi Aprili akisema kuwa suala hilo limeleta aibu kwa upande wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *