Mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Democratic, Hillary Clinton amesema kuwa anasikitika kuwaita mashabiki wa mpinzani wake wa Republican, Donald Trump kama kundi la watu wasiostahili heshima.

Katika taarifa kwa waandishi wa habari mgombezi huyo wa Urais kwa chama cha Republican alisema kuwa kuna Wamarekani wengi wanaochapa kazi kwa bidii wanaoamini kuwa wamepuuzwa na wanasiasa nchini.

Hata hivyo alisema kuwa ataendelea kukebehi watu wenye madharau ubaguzi wa rangi.

Donard Trump
Donard Trump

Meneja Mkuu wa kampeni wa Trump alikuwa amemlaumu Clinton kwa kile alichokitaja kama matusi dhidi ya mamilioni ya raia wa Marekani aliposema kuwa wale wanaomwunga mpinzani wake walikuwa wabaguzi wa rangi, wapinzani wa kijinsia, maadui wa wapenzi wa jinsia moja na wanaochukia Waislamu.

Hillary Clinton na Donard Trump wanatarajia kupambana vikali katika uchaguzi mkuu ujao nchini Marekani ambapo kwasasa poande hizo mbili zinatupiana maneno katika kampeni za uchaguzi huo.

 Trump amekosolewa na baadhi ya wamarekani kutokana na kusambaza siasa chafu na za kibaguzi kwenye kapuni zake pamoja na kumchafua rais wa sasa wa Marekani Barack Obama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *