Benki Kuu ya Tanzania imesema Tanzania iko sawia katika muelekeo wa kufikia kukua kwa uchumi kwa asilimia 7.2 mwaka huu.
Benki hiyo imekanusha madai ya baadhi ya wabunge wa upinzani ambao wamedai kuwa uchumi wa nchi unayumba kadri siku zinapokwenda.
Taarifa iliyotolewa na Benki Kuu jana imesema kwamba inatarajia ongezeko kubwa la ukuaji wa uchumi katika kipindi cha mwaka 2016 hasa baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli kuidhinidha uwekezaji katika miondombinu, udhibiti wa ukusanyaji mapato na vita dhidi ya rushwa.
Benki Kuu imesema kutokana na viashiria mbali mbali na mwenendo wa uchumi ni dhahiri kuwa uchumi wa Tanzania uko katika hali nzuri na kuwa na matumiani ya kufikia lengo la ukuaji wa pato la ndani GDP kwa asilimia 7.2 kwa mwaka huu.