Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amezitaka nchi za Sudan Kusini na Burundi kudumisha amani kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ujumla.

Akitoa taarifa ya kikao cha dharura mara baada ya viongozi hao wa EAC kukutana jana Jijini Dar es Salaam Rais Dkt. Magufuli ametoa wito kwa nchi hizo zenye migogoro na machafuko kukaa pamoja kukubalina ili kudumisha amani katika mataifa hayo.

Rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir
Rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir

Dkt. Magufuli ametumia fursa hiyo kuitaka nchi ya Sudani kusini kuzitaka pande zinazopingana kuweka silaha chini kwa ajili ya majadiliano ili kuepusha vifo zaidi vinavyotokana na mgogoro huo uliosababisha vita katika nchi hiyo.

Aidha Rais Magufuli amesema kuwa taarifa ya mpatanishi wa mgogoro wa Burundi, Mhe. Benjamin Mkapa imetoa mapendekezo kadhaa ambayo yatasaidia kumaliza mgogoro huo ambao nao umesababisha wakimbizi wengi kukimbilia nchi nyingine za afrika mashariki.

Siku tatu nyuma rais Magufuli alipokea ujumbe maarumu kutoka kwa rais wa Sudani Kusini, Silva Kiir na rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza wakisema kwamba nchi zao kwasasa zimetulia na hazina tena fujo.

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza

Sudan Kusini inakabiliwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya rais Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake Riek Machar ambapo hadi sasa pande hizo mbili zinarumbana japokuwa Machar sasa hayupo nchini humo.

Burundi inakabiliwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe baada ya rais wa nchi hiyo kujiongezea muda wa kiutwala ambapo baadhi ya raia wamepinga kitendo hiko.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *