Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Gabon, Jean Ping amekata rufaa kwenye mahakama ya katiba kupinga matokeo yaliyompa ushindi rais Ali Bongo ambapo amesema aliibiwa kura kwenye uchaguzi uliopita.
Ping hakubaliani na matokeo hayo kutoka kwenye majimbo ya Bongo ambapo yeye alishinda kwa zaidi ya asilimia 95 ya kura zote ambapo waliopiga kura walikuwa ni asilimia 99.93.
Waangalizi wa umoja wa ulaya nao wamekosoa matokeo hayo kwa baadhi ya majimbo kwenye uchaguzi huo.
Ping amesema watu kadhaa wameuawa kwenye vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi lakini serikali imesema kuwa ni watatu pekee ndiyo waliuawa.
Kwa upande wake rais Ali Bongo amesema kwamba yeye yupo tayari kuhesabiwa upya kwa kura kama mahakama itaamuru ifanywe ivyo.
Rais Bongo ameanza kuiongoza Gabon toka mwaka 2009 baada ya kufariki baba yake Omar Bongo na kiti hicho kirithiwa na yeye.