Klabu ya Crystal Palace imemsajili kiungo wa zamani wa Arsenal, Mathieu Flamini ambapo amesaini mkataba wa mwaka mmoja mpaka mwisho wa msimu huu.

Flamini mwenye umri wa miaka 32 ameondoka Gunners mwisho wa msimu wa mwaka jana ambapo alicheza jumla ya mechi 246 na kushinda vikombe vitatu vya FA akiwa na Arsenal.

Flamini ambaye ni raia wa Ufaransa pia ameshinda taji la ligi kuu nchini Italia maarufu kama Seria A mwaka 2011 kupindi akiwa anachezea klabu ya AC Milan.

Flamini: Akishangilia goli wakati akiwa Arsenal
Flamini: Akishangilia goli wakati akiwa Arsenal

Flamini aliondoka Arsenal na kuelekea AC Milan baada ya kudumu miaka minne ndani ya klabu ya Arsenal kabla ya kurejea tena Emarates mwaka 2013.

Kocha wa Crystal Palace, Alan Pardew amesema kuwa usajili huo ni mzuri kutokana na kiungo huyo kuwa na uzoefu na ligi kuu nchini Uingereza kwa hiyo atakisaidia kikosi chake.

Wachezaji waliosajiliwa na Crystal Palace msimu huu ni, Andros Townsend, Steve Mandanda, James Tomkins na Christian Benteke pamoja na Loic Remy aliyesajiliwa kwa mkopo akitokea Chelsea na sasa wamemsajili na Flamini.

                                                                                                                Top of Form

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *