Michuano ya Olimpiki kwa watu wenye ulemavu imeanza jana mjini Rio de Janeiro nchini Brazil.
Moja ya changamoto kubwa katika michuano hiyo ya Olimpiki ni kugubikwa na mgogoro wa kifedha pamoja na mauzo ya tiketi za ufunguzi wa michuano hiyo kwenda mwendo wa kobe.
Michuano hiyo inatarajiwa kushirikisha wanariadha zaidi ya elfu nne kutoka mataifa mia moja na sitini ulimwenguni watakao kuwa katika gwaride la ufunguzi ingawa miongoni mwa hao wanariadha wa kutoka nchini Urusi hawamo.
Wanamichezo wa Urusi wamepigwa marufuku kushiriki michuano hiyo kutokana na wasiwasi wa utumizi wa dawa za kusisimua misuli ambazo zilipigwa marufuku michezoni.
Sherehe za ufunguzi wa michuano hiyo zimeshuhudiwa na mamilioni ya watu ulimwenguni kote.