Mshambuliaji wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic amechaguliwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi kupitia tovuti ya Eurosport kwa mwezi Agosti barani Ulaya.
Ibrahimovic alifanikiwa kupata kura nyingi zaidi ya wachezaji wengine ambao walikua anashindanishwa nao, hii ni baada ya viwango walivyovionyesha katika mwezi Agosti ambapo ligi kadhaa za barani Ulaya zimeanza.
Mashabiki 60,000 walishiriki kupiga kura kupitia tovuti ya Eurosports ambayo imeanzisha mchakato huo katika kipindi hiki cha msimu wa 2016/17. Ibrahimovich aliongoza kwa kupata alama 10, mbele ya mpinzani wake wa karibu Sami Khedira wa Juventus FC.
Orodha ya wachezaji walioshirikishwa kwa mwezi Agosti pamoja na matokeo ya kura zilizopigwa.
Zlatan Ibrahimovic (Manchester United) – 10 points
Sami Khedira (Juventus) – 9 points
Layvin Kurzawa (Paris Saint-Germain) – 8 points
Domenico Berardi (Sassuolo) – 7 points
Alexanre Lacazette (Lyon) – 6 points
Arda Turan (Barcelona) – 5 points
Robert Lewandowski (Bayern Munich) – 4 points
Marcos Asensio (Real Madrid) – 3 points
Raheem Sterling (Manchester City) – 2 points
Andre Schurrle (Borussia Dortmund) – 1 point
Mchakato huu wakupata mchezaji bora wa kila mwezi kupitia Eurosports, unashirikisha ligi tano kubwa za barani Ulaya ambazo ni Premier League (England), La Liga (Hispania), Bundesliga (Ujerumani), Serie A (Italia), Ligue 1 (Ufaransa).