Serikali ya Somalia imesitisha kwa muda ndege zote zinazoingiza miraa kutoka taifa jirani la Kenya na kuingia nchini mwao.
Biashara hiyo ina thamani ya mamia ya mamilioni ya madola kila mwaka ambapo Kenya ufanya Somalia kama ndiyo soko kuu la bidhaa hiyo.
Waziri wa maswala ya anga nchini Somalia, Ali Ahmed Jama Jangali amesema kuwa marufuku hiyo itaanza kutekelezwa siku ya Jumanne lakini hakutoa maelezo zaidi.
Miraa ni maarufu sana nchini Somalia ,ambapo hutafunwa kwa saa kadhaa na hutumika kusisimua mwili .
Miraa mingi katika sehemu ya kusini na katikati mwa Somalia hutoka nchini Kenya.
Miraa hutumika na imepigwa marufuku nchini Marekani pamoja na mataifa kadhaa ya Ulaya.