Mgombea wa urais nchini Marekani kupitia chama cha Republican, Donald Trump amezuru kanisa moja la watu weusi mjini Detroit katika jaribio la kuchukua kura za watu walio wachache kutoka kwa mpinzani wake wa chama cha Democrat Hillary Clinton.

Trump ameuambia umati wa watu kwamba anaelewa kwamba Wamarekani weusi wamekabiliwa na ubaguzi.

Kura za maoni zinasema kuwa Trump ambaye yuko nyuma ya bi Clinton kwa umaarufu ana ufuasi mdogo miongoni mwa Wamarekani weusi na wapiga kura wa Hispanic.

Katika ziara yake hiyo aliandamana na Ben Carson mgombea wa chama cha Republican ambaye alilewa katika mji huo.

Trump amekosa kuungwa mkono na wamarekani weusi kutokana na kali zake za kibaguzi anazoziongea katika mikutano yake ya kampeni katika maeneo tofauti nchini Marekani ambapo anaonekana kuwagawa raia wa nchi hiyo.

Mgombea huyo ambaye anawania kiti hicho cha urais kupitia chama cha Republican anachuana vikali na mgombea wa chama cha Democratic bi Hilaly Clinton kwenye uchaguzi mkuu nchini Marekani.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *