Umoja wa Mataifa umesema lazima zifanywe juhudi zaidi za kulinda uhuru wa vyombo vya habari nchini Somalia baada ya waandishi wa habari 30 kuawa katika miaka mine iliyopita.

Shirika la kutetea haki za kibinaadamu la Umoja wa Mataifa limesema katika ripoti yake kwamba tangu mwaka wa 2014 waandishi wa habari mia 120 wengine wamekamatwa kiholela.

Ripoti hiyo imetaka haki ya kujieleza iheshimiwe kabla ya uteuzi wa bunge jipya baadae mwezi huu.

Wabunge 18 wameuawa tangu 2012 na wanaharakati kadha wa kisiasa wamefungwa.

Waandishi wa wanasiasa wamekuwa wakiuawa na wapiganaji wa kundi la al Shabab pamoja na wapinzani ambao wanapinga kazi yao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *