Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya limesema kuwa limebaini kundi kubwa la vijana walio chini ya umri wa miaka kumi na minane kutumika katika matukio ya wizi pamoja na uporaji wa mali kwa wananchi kwa kutumia silaha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishna wa Polisi Zahiri Kidavashari amesema wamegundua jambo hilo katika opresheni maalum ya kupambana na uhalifu Mkoani humo.

Kamanda Kidavashari amesema jeshi hilo linawashikiliwa watu 25 kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo la wizi wa magari pamoja na uporaji wa mali kwa wananchi kwa kutumia nguvu na silaha.

Pia Kamanda huyo amesema kuwa wameamua kufanya msako huo maalum baada ya kuwepo kwa malalamiko ya wananchi wengi mkoani humo kulalamikia kuporwa mali zao pamoja na magari na kundi hilo la uhalifu ambalo wengi wao ni vijana.

Kwa upande mwingine aKamanda Kidavashari amesema jeshi hilo linawashilia watu 19 ambao wanadaiwa kununua mali za wizi huku wengine watu wawili wakishikiliwa kwa kosa la kukutwa na noti bandia zenye thamani ya zaidi ya shilingi laki tatu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *