Klabu ya Manchester City imekubali kumruhusu kiungo wake Samir Nasri kujinga na Sevilla kwa mkopo wa muda mrefu.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 anatarajia kuelekea Hispania kwa ajili ya kufanyiwa vipimo ili aweze kujinga na Sevilla.
Nasri ameshindwa kupata namba kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester City tokea awasili kocha wa klabu hiyo Pepe Gurdiola na kuamua kumtoa kwa mkopo kuelekea Sevilla ya Hispania.
Manchester City wanatarajia kumuuza moja kwa moja mchezaji huyo kwasababu hayupo kwenye mipango ya Pep Gurdiola.
Nasri anakuwa mchezaji wa pili kupelekwa kwa mkopo ambapo Joe Hart tayari anaelekea Torino baada ya kuwasili kwa kipa, Claudio Bravo kutoka Barcelona.