Shirika la viwango Tanzania TBS limekamata mabati elfu 57 yaliyo chini ya kiwango yaliyoingizwa nchini kutokea China na mfanyabiashara wa bidhaa hiyo jijini Dar es Salaam.

Afisa Viwango na Mkaguzi wa TBS, Yona Afrika amesema mabati hayo yatateketezwa na TBS kutokana na kutofikia viwango vya kuzuia kutu au vilivyo orodheshwa kwenye kiwango cha mabati cha namba 353 ya kiwango cha rangi kinachotakiwa kuwepo kwenye mabati na shirika la TBS.

Afisa viawango huyo amesema madhara ya kutumia mabati hayo yapo kiuchumi, ki mazingira, Kiafya na kiusalama hivyo amewataka wafanyabiashara wanaoingiza mizigo na bidhaa mbalimbali nchini kuhakikisha kuwa wanakidhi viwango vya shirika hilo katika kuingiza bidhaa nchini.

Kwa upande mwingine naye Ally Chacha aliyeongea kwa niaba ya mfanyabiashara huyo ameitaka serikali pindi inapobaini kuwa kuna bidhaa imekosa viwango vya ndani ya nchi kuwapa fursa wafanyabiashara kuhamisha bidhaa hizo kwenda nchi nyingine zinazohitaji bidhaa hizo kuliko kuwasababishia hasara kubwa kibiashara baada ya kuziteketeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *