Klabu ya Al-Ittihad Alexandria ya Misri imetangaza kuvunja mkataba na mchezaji wa kimataifa wa Cameroon, Samuel Nlend kutokana na kugundulika kuwa nyota huyo ana maambukizi ya HIV.

Al Ittihad Alexandria imevunja mkataba na Samuel Nlend mwenye umri wa miaka 21 kutokana na kupimwa kwa nyota huyo na kugundulika kuwa na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi.

Uwamuzi huo umekuja ikiwa ni siku nne zimepita toka nyota huyo asaini mkataba wa miaka mitatu wa kuichezea klabu hiyo.

Mchezaji huyo alisaini mkataba wa miaka mitatu wa kuichezea Klabu ya Al Ittihad Alexandria ya nchini misri.

Samuel Nlend: Akiwa na viongozi wa klabu ya Al-Ittihad baada ya kusaini mkataba wa kuichezea timu hiyo.
Samuel Nlend: Akiwa na viongozi wa klabu ya Al-Ittihad baada ya kusaini mkataba wa kuichezea timu hiyo ambayo sasa imevunja mkataba na mchezaji huyo.

Samuel amewahi kuichezea timu ya Taifa ya Cameroon mechi tano hata hivyo hakuna sheria yoyote itakayomzuia staa huyo kupata kibali cha kucheza soka katika klabu nyingine licha ya kugundulika kuwa na virusi hivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *