Mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Yanga SC na JKT Ruvu uliokuwa ufanyike Jumatano hii Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam umeahirishwa.
Sababu ya kuhairishwa kwa mechi hiyo inatokana na Yanga kuomba kuahirishwa kutokana na kuwa na wachezaji wengi katika kikosi cha Taifa Stars.
Wachezaji hao walioitwa Taifa Stars ni kipa Deogratius Munishi ‘Dida’, mabeki Vincent Andrew ‘Dante’, Kelvin Yondani na Mwinyi Hajji, kiungo Juma Mahadhi na mshambuliaji Simon Msuva.
Vile vile Yanga imesema wachezaji wake wengine, beki Vincent Bossou (Togo), kiungo Haruna Niyonzima (Rwanda) na mshambuliaji Amissi Tambwe (Burundi) nao wameitwa na timu zao za taifa na kufanya idadi ya wachezaji wanane.
Kanuni za Ligi Kuu ya Tanzania Bara zinaruhusu timu ambayo wachezaji wake wasiopungua watano wameitwa timu za taifa kuahrishiwa mechi.