Rais wa sasa nchini Gabon, Ali Bongo na mpinzani wake mkuu bwana Jean Ping kila mmoja anadai ameshinda kiti cha urais baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wa Rais siku ya Jumamosi.

Pande zote zimekuwa zikilaumiana kwa udanganyifu huku Jean Ping amewaambia wafuasi wake kwamba ameshinda uchaguzi huo na anamsuburi Rais anayemaliza muda wake kumpongeza.

Huku upande wa Rais Bongo umesema inaendelea na awamu nyengine madarakani kwa kushinda uchaguzi huo.

Kufuatia mvutano huo wa pande hizo mbili Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo amearifu kuwa si halali kwa mtu yoyote kutangaza matokeo isipokuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi pekee ndiyo yenye wajibu wa kufanya hivyo

Jean Ping kiongozi wa zamani katika Umoja wa Afrika anajaribu kuuondoa madarakani utawala wa Bongo ambao umekaa madarakani kwa karibu miaka 50.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *