Waimbaji wa Bongofleva kutokea lebo ya Wasafi, Zuchu na Mbosso ndio wasaniii wa muziki pekee Tanzania waliochomoza katika orodha ya vijana 100 barani Afrika waliokuwa na ushawishi mwaka 2022.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya Avance Media iliyotoka wiki hii ambayo imeangazia vijana 100 Afrika kutoka nchi 25 tofauti katika sekta mbalimbali kama burudani, biashara na uongozi.

Hata hivyo, majina makubwa katika muziki wa Bongofleva kama Diamond Platnumz, Alikiba, Rayvanny na Harmonize hajaonekana katika ripoti hiyo.

Nchi ya Nigeria ndio imetoa vijana wengi wenye ushawishi Afrika wakiwa 31, inafuatia Kenya 11, Ghana 10, Tanzania saba na Afrika Kusini watano. Miongoni mwa waimbaji wa Nigeria waliotajwa ni Wizkid, Burna Boy, Tems, Davido, Kizz Daniel, Fireboy DML, Asake, Ckay, Omah Lay, Mr. Eazi na Rema.

Kwa ujumla Watanzania saba waliotajwa katika ripoti hiyo ni Zuchu, Mbosso, Kili Paul, Jokate Mwegelo, Millard Ayo, Benjamin Fernandes na Barbara Gonzalez.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *