Meneja wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka na kuweka wazi kuwa wimbo mpya wa Diamond ‘Zuwema’ ulirekodiwa miaka minne nyuma.

Kupitia akunti ya Instagram Babu Tale ameanza kwa kuandika ‘Kinginge ambacho hamkijui kwenye huu wimbo Zuwena nikwamba umerekodiwa miaka minne (4)I liopita yani mimi na wenzangu Mkubwa Fella na Sallam SK tumeusikiliza mpk tukaukatia tamaa kua hautatoka, niliwahi kumtafuta Lamata awe Director wa huu wimbo na alikua tayari.

Pia ameendelea kuandika tatizo lilikua kwa mwanamziki mwenyewe alidai muda wahuu wimbo kutoka bado. na ikiwa tayari nitakwambia Boss.

Pia aliendelea kwa kuandika Bas mwezi mmoja nyuma kanambia huu ndio mwaka wa ZUWENA kutoka na nitaidirect mwenyewe. niliogopa kwakua niliona wimbo umekaa sana ndani.

So nikweli utafika Kule tunapotaka ufike? Ghafla wimbo umefika na umekua mkubwa Africa. Kuna chakujifunza hapa. KIZURI NIKIZURI TU HATA UKIFUNIKE NA GUNIA. niwaibie siri. bado zingine mbili nazo zilirekodiwa miaka saba (7) iliopita naamini zitapokelewa vizuri pia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *