Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize ameweka wazi kuwa kwasasa hana hisia za kupenda tena licha ya kutokea wasichana wengi wanaotamani kuwa nae kwenye mahusiano.
Harmonize ameandika “Wanawake wengi wazuri wamejitahidi kunishawishi kupenda tena kwasababu wanajua ninapopenda nakuwa rafiki,mume, mtoaji na baba bora, nalikubali hilo.
Pia ameendelea kuandika “Lakini moyo wangu kwa sasa hauko tayari kupenda kabisa. Natumaini sitokuwa hivi daima. Niombeeni ili moyo wangu uweze kuruhusu kupenda tena”
Swala la kuingia kwenye Mahusiano tena limekuwa mtihani sana kwa mwanamuziki huyo ni kama vile amekata tamaa na mahusiano baada ya kuachana na Kajala.