Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Aslay amemmpa ushauri mrembo Amber Lulu huku akimsisitizia aachane na mambo ya trending bali afanye muziki na kumlea binti yake ambaye ni kama mama yake.
Aslay amemshauri mambo mengi huku kubwa kabisa akimshauri amlee mtoto wake kwasababu huyo ndiye mama yake aliyebaki lakini pia aachane na mambo ya kutaka kutrend maana alishafanya hivyo vitu sana hivyo aendelee kufanya muziki tu kama riziki yake ipo basi itakuja.
Amber Lulu amepost meseji hizo kupitia Instastory yake na kuandika ‘Asante Ndugu Yangu Limenijenga Sana Na Umenikumbusha Mbali’.
Mara ya mwisho Amber Lulu kuzungumziwa sana mtandaoni ilikuwa ni mara baada ya kuweka picha zake zinazomuonyesha akiwa na majeraha ya kupigwa vibaya na akilalamika kuchoshwa na vipigo hivyo japo hakuweka wazi mtu aliyemfanyia hivyo lakini watu wengi walimshutumu baba wa mtoto wake.