Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Linex amempngeza msanii mwenzake, Dayoo kwa ubunifu wake alioufanya kupitia wimbo wake mpya ‘ Moyo’ huku akiuita Upendo Wa Kweli.
Kupitia wimbo huo Dayo kuna sehemu anasikika akiitaja saini ya Linex ‘Jejejeida’ kitu ambacho kimemfanya Linex ashangae mpaka kuandika kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Ameanza kwa kuandika ‘Hii ni true love gani alioneshwa Huyu mdogo wangu Dayo Enzi Za Jejejeida ??? Any way Jejeida Still am here naiwakilisha kitaa Yangu KIGOMA ili Dude La Dayo link ipo kwa bio yake’.
Hii si mara ya kwanza kwa msanii kuja na ubunifu wa namna hii katika nyimbo lakini si mara zote watu waliotajwa kwenye nyimbo husika hujibu namna hii.