Meneja wa muziki nchini Tanzania, Mkubwa Fella ambae pia ni mmoja wa Mameneja kutoka Record Label ya WCB amefunguka kwa undani wake kuhusiana na Mchango wake kwenye Game ya Bongo Fleva.

Sehemu ya Mahojiano hayo Fella anasikika akisema “Nimetengeneza ajira na mimi ndiye Meneja wa kwanza wa wasanii hapa nchini Nakosaje tuzo Hapa Tanzania.

Mimi ndiye niliebuni huu Umeneja wa wasanii Mpaka leo sijapewa tuzo Nimewasaidia vijana wa Kitanzania Leo wamefanikiwa Wananiona wanadharau.

Fella alianza umeneja baada ya kuwaongoza wasanii mbali mbali wakiwemo Juma Nature, Temba, Chege Pamoja na kundi la Yamoto band lililokuwa linaundwa na wasanii wanne ambao ni Aslay, Beka Flavour, Mbosso na Enock Bella.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *