Baada ya ‘Follow Me’ aliyoshirikiana na Harmonize na ‘Mouzzah’ kutoka miezi miwili iliyopita, nguli wa muziki nchini Tanzania, Aslay ameachia kazi yake mpya iitwayo ‘Inauma’.
Nyimbo ambayo inaanzisha Mwaka 2023 kwenye muziki wake japo ukimya wake wa muda mrefu uliwatia hofu mashabiki zake lakini kwa mwendelezo huu tayari imani ya mashabiki imerudi na burudani inaendelea
Aslay kwa sasa yupo chini ya lebo kubwa ya muziki Afrika ijulikanayo kama Sony Music Africa na kazi zake zikisimamiwa na Rock Star Africa.
Mwaka 2023 ni mwaka mwingine wa Aslay kukonga mioyo ya mashabiki zake na wapenzi wa muziki wake.