Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Peter Msechu amekuwa miongoni mwa watu waliopatiwa matibabu ya kuwekewa puto tumboni (intragastric balloon) katika hospitali ya Mloganzila, Dar es Salaam.

Msechu mbali na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha huduma za afya nchini pamoja na viongozi wote wa Serikali wanaohusika na sekta hiyo, amewaambia Watanzania wategemee mabadiliko makubwa.

“Leo ni siku ya kipekee kwanza kiafya na maendeleo binafsi kama binadamu ambaye ninahitaji afya njema baada ya kupambana muda mrefu kwa mazoezi na diet.

Naishukuru Serikali chini ya Rais Samia kwa kutuletea huduma ya kuwekewa puto tumboni.

uduma hii inafanyika kwa uweledi mkubwa na mimi nipo rayari kupata puto langu,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *