Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole ametangaza kuvunjwa kwa Mgahawa wake Tawi la Dar es Salaam kwa sababu za kupisha ujenzi wa Kituo Cha Afya.
Shilole amefunguka kuwa alipewa eneo hilo na Manispaa ambapo kwa kipindi hicho lilikuwa ni eneo la wazi lakini sasa wameamua kujenga kituo cha afya kwa ajili ya wananchi wa Kinondoni.
Shilole amesema kuwa atatangaza eneo lingine ambalo pia amepewa na Serikali kwa ajili ya biashara yake hiyo ya chakula ambayo ni maarufu.
Shishi Food anamiliki migahawa hiyo ya chakula sehemu mbali mbali nchini ikiwemo mikoani kama vile Dodoma na sehemu nyingine ambapo anafanyia biashara hiyo.