Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Kusah amefunguka na kusema kuwa hawezi kujiunga na lebo za hapa nchini kwakuwa hawana uwezo wa kumlipa pesa anayotaka.
Kusah amesema kuwa hawezi kwani hawana uwezo wa kumlipa watadanganyana tu na kukazia kuwa labda kwa lebo kubwa za nje kama Universal Music Group na Sony Music ataweza kukubali kusajiliwa.
Mwanamuziki huyo ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa albam ya mwanamuziki wa Bongo Fleva ambaye kwasasa ni mbunge, Keisha.
Lakini amedokeza kuhusu kufunga Ndoa na Aunty Ezekiel kuwa kitambo wamefanya hivyo na alipoulizwa ndoa ya mkeka akasema ndoa ni ndoa tu.