Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marioo amefunguka na kusema kuwa kwasasa anatarajia kupata mwanamke kwa ajili ya kuanzisha nae mahusiano.

Marioo kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram amevunja ukimya kwa kudai kuwa sasa anahitaji Mwanamke wa kuishi nae Kwenye Jumba lake la Kifahari.

Marioo inaonekana amechoka kuwa Singo mpaka kufikia hatua ya Kutafuta mwenza yani hapa Zile tetesi za kusema kuwa yupo kwenye Mahusiano sio kweli kulingana na Anacho kipitia Muda huu Toto Bad amesema kuwa “Jumba kubwa kama Hili linahitaji Mwanamke bila mwanamke ni kama Hall tu” Aliandika Marioo.

Lakini pia Marioo aliendelee kupigilia msumali kwa kuongeza Chapisho lingine ambapo linasema kuwa ” Aisee najiona kabisa Nahitaji mwanamke mzuri mwenye akili.” – Marioo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *