Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Amber Lulu ameeleza kunyanyaswa au kufanyiwa ukatili wa kipigo kwenye mahusiano yake.

Amber ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kike aitwaye Ariana aliyezaa na msanii Bosheni ameelea kuumizwa vibaya kwa kipigo katika mwili wake.

Kwa mujibu wa Amber Lulu, chanzo kikubwa cha kipigo hicho ni mtoto wake huyo bila kufafanua.

Ameandika; “Daa nimekuwa mtu wa kuhangaika na kuteseka pasipo sababu ya msingi, mapenzi niliyinayo kwa mtoto wangu na uchungu na uvumilivu, Mungu pekee ndiye anajua.

“Kuna muda najitoa nafanya chochote kwa ajili ya mwanangu na nilizaa kwa mapenzi na mapenzi ya Mungu naona ila ninachofanyiwa kama sina haki kuna muda natamani kumkumbatia mwanangu nishinde naye nashindwa cos nisipohangaika mtoto wangu atakula nini?

Nyumba nalipa mimi, leo napigwa kama mbwa kisa kumhangaikia mwanangu, naumia sasa hivi mtu anatishia kuniua.“Mpaka naogopa kurudi nyumbani kwangu, mtoto wangu namuita hoteli, ukiangalia mwili wangu kama daah.

Si mara ya kwanza kwa Amber Lulu kulalamika kupigwa na mwanaume, lakini amekuwa hachukui hatua yoyote dhidi ya ukatili huo wa kijinsia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *