Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marioo ametangaza show yake ya kwanza kubwa ndani ya mwaka 2023 katika Ukumbi wa Mlimani City Dar Es Salaam.
Show hiyo ambayo itafanyika 28 Mwezi huu itakuwa ni show yake ya kwanza ya aina yake kutokana na muimbaji huyo kuwa na nyimbo bora nyingi.
Marioo ni msanii anayefanya vizuri kwa sasa huku baadhi ya wadau wakidai kwa sasa ameanza kuwa tishio kwa wasanii wengi ambao wanadaiwa kuongoza game.
Producer maarufu nchini Abbah ambaye anafanya kazi na msanii huyo amewahi kunukuliwa kwamba lengo la msanii huyo ni kwenda taratibu kimataifa kupitia muziki wake kitu ambacho tayari kimethibitika.
Wimbo kama Mi Amor ni moja kati ya nyimbo za wasanii wa Tanzania zilizotokea kwenye chart za nyimbo zilizosikilizwa na kutengeneza gumzo duani.