Aliyekuwa mke wa mwanamuziki wa Tanzania, Ben Pol aitwae Anerlisa ameonyesha kutofurahishwa na kile ambacho alikizungumza Ben Pol Kuwa Hajawahi Kufurahishwa na ndoa yake na mrembo huyo.

Anerlisa anashangaa ni kwanini Ben kila siku amekuwa akiongea mambo mengi ili mrembo huyo aonekane mbaya lakini pia amemtaka Ben Pol aache kumuongelea kwani yeye pia ana mengi kumuhusu lakini amechagua kukaa kimya kama mwanamke.

Kupitia InstaStory yake Anerlisa ameweka jumbe mbili tofauti ya kwanza ikisomeka “Ben naona umenizoea na unachukulia ukimya wangu kama udhaifu wangu. Ulikuwa na uwezo wa kumwambia anaekuhoji asikuulize kuhusu mimi. Kwa nini unapenda kila mara mimi nionekane mbaya. Chini ya kapeti unanitumia jumbe tofauti tofauti na namna unavyoniongelea”.

Na ya pili inasomeka “Kama kweli wewe ni mwanaume, nakuomba uweke wazi jumbe zote ulizokuwa unanitumia tangu Desemba 25 hadi Januari 4, 2023. Nina mengi ya kuzungumza kuhusu wewe au kuonyesha, lakini nimechagua kusimama kama Mwanamke.” “Ni rahisi sana, acha kuniongelea.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *