Mwanamuziki na mtangazaji wa Radio, Baba Levo amefunguka na kusema kuwa mwanamuziki, Marioo alikosea kusema kuwa hajawahi kutaka kusainiwa na WCB.

Baba levo amesema kuwa Diamond amechukizwa na kauli ile ya Marioo na inaonyesha Marioo amemuambia Diamond muongo wakati ilikuwa kweli alichoongea.

Baba Levo anasema kuwa kwa kile alichosema Marioo kwa upande wake hadhani kama Collabo ya Marioo na Diamond ambayo tayari ilisharekodiwa kama itatoka.

Siku kadhaa zilizopita mwanamuziki, Diamond alisema kuwa alifuatwa na Marioo kutaka kujiunga ndani ya lebo ya WCB kauli ambayo Marioo aliipinga vikali kwa kusema sio kweli.

Marioo alisema kuwa kwa upande wake hakuwahi hata siku moja kumfuata Diamond kwa ajili ya kumuomba ajiunge na lebo ya WCB.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *