Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuchu amewaomba radhi wapenzi wa Muziki nchini Kenya na Mashabiki wake kwa ujumla kufuatia Kuahirishwa kwa Show zake Mbili nchini Kenya.

Zuchu alitakiwa kufanya Show mbili nchini Kenya ambapo Show ya kwanza ilitakiwa kufanyika Jumamosi Tarehe 10 kwenye Ukumbi wa Racecorse Waterfront huku Nyingine ilitakiwa kufanyika Siku ya Jumapili Disemba 11/2022.

Kupitia ujumbe wake Zuchu amesema kuwa amesikitishwa na kuhairishwa kwa show zake Mbili nchini Kenya kwani ni Jambo ambalo lilikuwa nje ya uwezo wake Zuchu aliongeza kwa kusema kuwa Taarifa njema ni kwamba Mapromota wake watatangaza tarehe Mpya za Show.

Mashabiki ambao walinunua Tiketi za show hizo Tiketi zao zitasalia kwenye Show ijayo au vinginevyo watarudishiwa Pesa zao.

Aidha Zuchu alimaliza kwa kuwaomba radhi Mashabiki wake kwani ni jambo ambalo lipo nje ya Uwezo wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *