Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed maarufu kama ‘Shilole ‘ ameamua kuwahamasisha mastaa na watu mbalimbali nchini.
Shilole amewataka mastaa hao kuepuka gharama ya kujitengeneza badala yake wanaweza kubaki na uhasili wao na wakapendeza.
Shilole alisema, amejitathmini na kugundua kuwa hatumii gharama kubwa kununua nywele za bei mbaya au kutumia madawa ya usoni, lakini bado anaonekana mrembo.
“Ukitaka kuniangalia kuanzia kichwani hadi ngozi yangu situmii gharama hata kidogo, naamini mastaa wengine wakiamua kuwa jinsi walivyo watapendeza na wataepuka gharama ambazo si za muhimu,” alisema Shilole.