Mwanamuziki wa Bongo Fleva Harmonize ameomba radhi kutokana na maudhui ya wimbo wake mpya wa Weed language ambao umekiuka maadali na tamaduni za Kitanzania.

Kupitia Insta Story yake Harmonize pamoja na uongozi wake wameomba radhi na kueleza kuwa wameamua kuuondoa wimbo huo kwenye platform zote za muziki na watajitahidi kutunga nyimbo zitakazoendana na maandili na tamaduni za Kitanzania.

Harmonize ameandika “Uongozi wa konde music worldwide unaomba radhi kutokana na maudhui ya wimbo tulioutoa hivi karibuni unaoitwa ‘WEED LANGUAGE’.
Wimbo huu ulilenga kupanua na kukuza muziki wetu nje ya mipaka ya nchi yetu

Lakini tafsiri ya maudhui ya wimbo huo yanakiuka maadili utamaduni, mila na desturi pamoja na miongozo ya mamlaka za serikali nchini.

Kutokana na kadhia iliyosababishwa na maudhui ya wimbo huo tunaomba radhi na tunahaidi kuuondoa wimbo huo kwenye mitandao yote ya kijamil.

Pia tunahaidi kuboresha nyimbo zetu ili ziendane na utamaduni wetu pamoja na miongozo ya mamlaka ya serikali. Imetolewa na uongozi wa konde music worldwide”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *