Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Juma Jux amekanusha kutoka kimapenzi na Paula ambaye ni mtoto wa staa wa uigizaji Bongo, Kajala Masanja.

Jux ameweka maneno sawa kuhusu kile kinachodhaniwa kuwa ni uhusiano wa kimapenzi baina yake na Paula.

Jux anasema kuwa uhusiano wake Paula ni wa kibiashara tu na wala hawajawahi kuvuka mipaka na kuzama kwenye penzi hata siku moja.

Staa huyo anaitetea video ambayo ilidaiwa kuwa Paula alionekana akiingia nyumbani kwake ambapo anasema kuwa hata hajawahi kufika katika makazi yake.

Jux anasisitiza kwa kumtaja Paula kama dada yake mdogo na wala hawezi kuingiwa na suala la kumuomba kuwa wapenzi.

Jux amesema kuwa kwa yupo kwenye uhusiano mwingine ambao unampa amani ya akili kupita maelezo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *