Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka ameshea ujumbe huu kwenye page yake ya Instagram baada ya ukimya wa muda mrefu kwenye mziki.
“Ni muda mrefu umepita, mengi yalizungumzwa lakini sasa ni wakati sahihi wa mimi kuzungumza”. ameandika Aslay.
Msanii huyo ambaye ni muandishi na producer pia kwa sasa amesainiwa lebo ya Sony Music Africa na kusimamiwa na Rock Star.
Mwanamuziki huyo aliyekuwa ana unda kundi la Yamoto Band amekuwa kimya kwa muda mrefu bila ya kuachia nyimbo yoyote.