Habari za mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize kumsaliti mchumba wake, Kajala Masanja baada ya kuvuja kwa video ya jamaa huyo akiwa na aliyekuwa mpenzi wake (ex), mrembo Briana nchini Australia.
Harmonize amefunguka kuwa, video hiyo ilikuwa ya kitambo na si kweli kwamba amechepuka hivi karibuni.
Video hiyo ni ya wimbo wake wa The Way You Are unaopatikana kwenye albam yake mpya ya Made For Us.
“Ni video yakitambo, iliachiwa kimakosa. Timu yangu inashughulikia jambohilo. Mwanaume mnene aliye kwenye video hiyo siyo mimi,” amesemaHarmonize.
Konde Boy anamsifia mchumba wake Kajala kwa kuhakikisha kuwa ana mabadiliko katika umbo lake.
“Mwili wangu una afadhali, mke wangu alinifanyia jambo, asante mpenzi wangu. Hakuna ninaloweza kufanya kuhusu mambo ya zamani,” anasemaKonde Boy.
Hata hivyo, Harmonize anawakejeli wapenzi wake watatu wa zamani akiwemo Briana katika wimbo wake wa My Way.
Katika wimbo huo, Harmonize anawashambulia wapenzi wake watatu wa zamani, Wolper, Sarah na Briana na anamsifia mchumba wake wa sasa ambaye ni Kajala.