Mwanamuziki wa Bon Rayvanny ametunukiwa Tuzo ya heshima kama msanii wa Afrika anayefanya vizuri duniani usiku wa kuamkia kwenye Tuzo za DIAFA zilizotolewa Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.
Baada ya kupokea tuzo hiyo Rayvanny aliwashukuru DIAFA na kueleza namna alivyoipokea kwa ukubwa Tuzo hiyo na kutangaza kui-dedicate kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
“Hii ni heshima kubwa ambayo DIAFA mmenipatia, si kwangu tu bali kwa Afrika nzima…. Nataka kuitoa Tuzo hii kwa Rais wangu, ni Rais wa kwanza mwanamke kwenye Taifa letu,” amesema Rayvanny.
Tuzo za DIAFA zilianzishwa Dubai mwaka 2017 kwa lengo la kuwatunuku kila mwaka Watu Mashuhuri kutoka Mataifa mbalimbali waliofanya kazi kubwa na kupata mafanikio ambapo Mwigizaji wa Pakistan Maya Ali ni miongoni mwa walioshinda Tuzo za mwaka huu.