Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja amefunguka na kusema kuwa ndoa yake na Irene Uwoya ilikuwa ndoa halali kabisa tofauti na watu wanavyofikiria.

Licha ya Arusha anakotoka kuwa na historia ya kutoa wanamuziki wengi, wazuri wa kitaifa na kimataifa, lakini aliibuliwa na kijana kutoka Manzese jijini Dar, Madee.

Madee alikuwa katika ziara ya kawaida ya kimuziki jijini Arusha miaka kadhaa iliyopita, lakini akashangazwa na kipaji cha msanii huyo ambaye kimsingi, alipaswa kuwa darasani shule ya msingi akisoma.

Madee alipomchukua Dogo Janja na kutinga naye jijini Dar na kumpa nafasi ya kuonesha kipaji chake, kweli kijana huyo wa Arachuga akaonesha umahiri mkubwa na kila mmoja akamkubali. Dogo Janja ameingia kwenye gemu kirahisi sana katika umri wake mdogo.

Ndani ya Lebo ya TipTop Connection, Dogo Janja alikuwa ndiye msanii mdogo kuliko wote na kazi ambayo aliifanya ilionesha ubora wa hali ya juu kiasi cha kugeuka lulu.

Kuna wakati, baadhi ya watu wakaanza maneno ya kumsema Madee kuwa alikuwa akimtumia dogo huyo kupiga hela. Walikuwepo hadi watu waliomfuata Dogo Janja mwenyewe na kumweleza kuwa ananyonywa.

Watu wengi walikuwa upande wake alipotangaza kuondoka, wakiamini alipaswa kufaidika kwa kipaji chake.

Ni kitu cha kawaida katika kazi yoyote, changamoto ni nyingi katika maisha hivyo halikuwa jambo la ajabu baada ya kujifunza, akarejea tena TipTop Connection na kuendelea na mzigo.

Hata hivyo, baada ya kupita kipindi kirefu, Dogo Janja ambaye jina lake halisi ni Abdulaziz Abubakar amefichua kile kile kilichotokea kati yake na Uwoya mwaka 2017.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *